-Niwapongeze watendaji na Menejimenti ya halmashauri kwa kazi kubwa mnayoifanya ya ukusanyaji wa mapato na usimamizi mzuri wa matumizi ya mapato hayo katika kuimarisha huduma kwa wana-nchi
- Ninyi ndo think tank la halamshauri Niwasisitie watendaji wote kuhakikisha mnaharakisha fursa za uwekezaji na biashara ndani ya halmashari
-Wanaohusika na utoaji wa vibali na usharuri hakikisheni nyaraka zinapowafikia mnazishughulikia kwa muda mfupi na kuzitolea maamuzi ili isiwe kikwazo kwenye uwekezaji na biashara.
- Kwa Maendeleo ya Mkoa na halmashauri zote nasisitiza kuongeza wigo kwenye utawala na usimamizi wa rasilimali watu na fedha zilizopo ili kila mmoja atimize wajibu wake
-Nina agiza Kila moja atimize wajibu wake katika kusimamia masuala ya utawala na usimamizi wa rasilimali watu na fedha kwa Maendeleo ya Mkoa na halmashauri zote
- Nasisitiza kupunguza hoja za Ukaguzi wa ndani au kuzimaliza kabisa na tujitahidi kuacha shughuli zote zinazosababisha uwepo wa hoja katika majukumu yetu ya kila siku .
-Halmashauri ziwe na utamaduni wa ndani wa kuwapongeza wafanyakazi wanaofanya vizuri badala ya kusubiri sherehe za Kitaifa ili kujenga morali ya ufanyaji wa kazi kwa bidii.
-Tupunguze migogoro ya ardhi kwa kushughulikia mashauri mbalimbali yanayohusiana na ardhi ili ardhi iweze kutumika kwenye uwekezaji na shughuli nyingine na kuongeza mapato ya halmashauri.
-Halmashari zihakikishe zinatoa elimu na mafunzo kwa Madiwani ya kuongeza ubunifu kwenye masuala ya uchumi, ubunifu wa miradi na jinsi ya kushirikiana na wawekezaji na wafanyabiashara kwenye halmashauri na Kata zetu.
-Suala la utengaji wa asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake.Vijana na watu wenye ulemavu ni lazima sio utashi wa mtu , ninasisitiza Halmashauri zote kuhakikisha zinatii agizo hilo na kupunguza malalamiko ya wanavikundi kwenye utoaji wa mikopo
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.