Waziri wa Sanaa, utamaduni na michezo Mhe. Mohamedi Mchengerwa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu na mikono awamu ya pili yajulikanayo kama NDILE MEYA CUP yanayotarajia kufanyika Julai 9 mwaka huu katika viwanja vya Nangwanda Sijaona vilivyopo Manispaa ya Mtwara-mikindani.
Akizungumza na waandishi wa habari Juni 30, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani mwanzilishi wa mashindano hayo ambae pia ni mstahiki Meya wa Mnaispaa hii Bi. Shadida Ndile amesema kuwa mashindano hayo yatahusisha timu kumi na nane za mpira wa miguu kutoka kata kumi na nane zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani na timu sita za mpira wa netiboli.
Mstahiki Meya amefafanua kuwa katika mashindano hayo anatarajia kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu hivyo amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kushiriki ligi hiyo.
Aidha amewaomba wadau mbalimbali wa michezo kujitokeza ili kumuunga mkono kwenye jambo hilo ili aweze kutimiza malengo aliyojiwekea ikiwemo kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye sena ya watu na makazi , kukutanisha vijana na kuimarisha upendo,kuwezesha vijana kukutana Pamoja na kubadilishana mawazo juu ya fursa mbalimbali za kiuchumi.
Malengo mengine ni pamoja na kuibua vipaji na kuwatafutia njia kuelekea kushiriki kwenye timu kubwa pamoaja na kuhamasisha michezo kwa jamii.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.