Ili kukuza uwezo wa kufikiri kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu nchini Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesambaza vifaa vya masomo na michezo vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.5 kwa wanafunzi hao walioko katika Mikoa yote nchini.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa kwa wanafunzi hao iliyofanyika Julai 17,2020 katika viwanja vya Shule ya Msingi Shangani , Mratibu wa Elimu maalumu kutoka Wizara ya Elimu Bwana. Omari Mkally amesema kuwa Wizara hiyo ina utaratibu wa kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa vifaa kwa wanafunzi hao
Amesema kuwa Jumla ya shule zipatazo 750 zenye kupokea wanafunzi wenye mahitaji maalumu nchini zimepokea vifaa hivyo na kusema kuwa utaratibuu huo ni endelevu tangu Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani.
Bi Juliana Manyama Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani ameishukuru Wizara ya Elimu kwa msaada walioutoa na kuwataka wazazi na walezi wote wenye Watoto wenye mahitaji maalumu kutambua kuwa wana haki sawa kama Watoto wengine ikiwemo kupata Elimu hivyo wasiwafiche.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.