Kamati ya Huduma ya Mikopo ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani inafanya ziara kutembelea na kufanya tathmini ya Uchambuzi wa maombi ya mikopo kwa vikundi vyote 169 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu vilivyokidhi vigezo vya awali kupatiwa mkopo huo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bwn. Mipawa Majebele alisema, Jumla ya maombi 190 yenye thamani ya Tsh. 3,463,853,080.00 yaliyopokelewa na Ofisí Kuu ya Halmashauri kupitia ldara ya Maendeleo ya Jamii ambapo Vikundi vya wanawake 126, Vijana 58 na Watu wenye Ulemavu 6.
"Baada ya kupokea maombi hayo Kamati za Mikopo Ngazi ya Kata zilitembelea vikundi vilivyoomba mikopo na kufanya tathimini. Taarifa ya tathimini ya kata inaonesha kuwa vikundi 169 vimekidhi vigezo vya kupatiwa mikopo yenye thamani ya Tsh. 1, 526,434,000 kati ya Tsh 800,000,000.00 zilizotangazwa kwa ajili ya utoaji wa mikopo kwa robo ya kwanza 2024/2025," alieleza.
Halmashauri ilitoa tangazo kwa umma juu ya uwepo wa fedha zilizotengwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu tarehe 25 Oktoba, 2024.
Kufuatia tangazo hili walengwa wa mikopo hii wameomba mikopo hiyo kupitia mfumo wa kielektroniki unaotambulika kama Wezesha Portal.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.