VIJANA WAHAKIKISHIWA KUPEWA MKOPO WENYE RIBA NAFUU
Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani Bi. Beatrice Dominic amewahakikishia vijana waishio Manispaa kuwa kama watajiunga kwenye vikundi na kujisajili atawapatia mkopo wenye riba nafuu.
Amesema kuwa fedha za kuwakopesha vijana zipo changamoto kubwa ni vijana hao kutojitokeza kwenye maombi ya mikopo na hivyo kupelekea fedha nyingi kukopeshwa kwa vikundi vya Wanawake. Aidha amesema anatambaua vijana hao wanashughuli nyingi za kufanya lakini kwa kuwa wameshindwa kutambua fursa walizonazo wamejibweteka kwa madai kuwa hawana mtaji wa kuweza kuwainua.
MKurugenzi ameyaongea hayo jana Novemba 3, 2017 kwenye uzinduzi wa jukwaa la vijana lililofanyika kwenye Ukumbi wa vijana uliopo tarafa ya Mikindani katika Kata ya Mtonya
Aidha amewataka vijana hao kutambua kuwa Mji wa Mtwara una fursa nyingi kwa sasa hivyo vijana wakizitambua na kuzitumia fursa zilizopo vizuri wataweza kujitegemea. Amezitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na uwepo wa mikopo kwa ajili ya kuwakopesha vijana na Wanawake,Sehemu ya Utalii Mikindani
Amebainisha kuwa kuna sababu nyingi zinazopelekea vijana kutofikia malengo yao ikiwa ni pamoja na kuwa na uoga wa kuthubutu hivyo amewataka kufanya kazi bila uoga, Uvivu pamoja kujutia kitu ulichosomea.
Hata hivyo amewataka vijana kutenga muda muda wa ziada wa kukaa pamoja hasa kwa wale wanaotaka kufanya shughuli zinazofanana na kuunda kikundi kimoja,,Kubainisha mahitaji na kwamba hadi kufika Disemba apate taarifa ili awapatie mafunzo na mikopo ambayo itasimamiwa na halmashauri.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vijana hao Salumu Ngauja amemuahidi Mkurugenzi kuwa hadi tarehe 25 Novemba atapeleka taarifa ya vikundi vilivyoundwa ambayo itaonesha shughuli wanazozifanya.
Nae Afisa Maendeleo ya Jamii John Samo amewakumbusha vijana kuwa changamoto kubwa inayoikumba halmashauri kwenye masuala mazima ya mikopo inayokopeshwa kwa vijana ni kuwa vijana hawarejeshi mikopo.
Awali akisoma risala kwa niaba ya vijana wenzake Farida Ahmadi amesema kuwa Jukwaa la vijana lilianz ana vijana 264 lakini hadi sasa wamebaki vijana103 nakwamba vijana wengi wamejitoa kutokanan na kutokuwa na uvumilivu. Aidha ameahidi wao kama vijana wako tayari kufanya kazi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.