Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amewataka Mafundi wenyeji (Jeshi la Magereza Mkoa wa Mtwara) waliopata kazi ya ukarabati wa miundombinu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara kufanya kazi kwa ufanisi ikiwemo kuwa na mpangilio wa kazi utakawaongoza ili waweze kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
Amesema kuwa kwa kuwa taasisi hiyo ni ya Serikali na ina nguvu kazi ya kutosha hivyo anatarajia kazi hiyo itafanyika kwa umakini na kwa uharaka ili shule zitakapofunguliwa wanafunzi waweze kuendelea na masomo.
Byakanwa ameongea hayo May 19,2020 alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi katika Shule ya Sekondari ya wasichana Mtwara na vyuo vya Ualimu vilivyopokea fedha za Ukarabati wa miundombinu kutoka Serikali Kuu.
Februari,15,2020 Shule ya Sekondari ya wasichana Mtwara imepokea fedha shilingi Milioni 776.7 kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya madarasa, mabweni Pamoja na majengo mengine.
Zoezi la ukarabati wa miundombinu katika shule hiyo limeanza Mei 1,2020 na linatarajia kukamilika ifikapo Julai 30,2020.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.