Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amesema kuwa katika msimu wa korosho wa mwaka huu, Bandari ya Mtwara inatarajia kusafirisha tani 11,000 za korosho na kuwataka wafanyabiashara mbalimbali Pamoja na wananchi kuchangamkia fursa hiyo.
Amesema kuwa meli tayari kwa ajili ya kubeba korosho imeshaweka nanga katika bandari hiyo.
Kyobya ameyasema hayo Novemba 1,2020 katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Stella Maris kilichopo Mtwara alipokutana na wafanyabiashara mbalimbali waliopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Aidha Kyobya amewataka wafanyabaishara hao kutumia mitandao ya kijamii kama vile whatssap, instragram na facebook katika kutangaza biashara zao.
Pamoja na hayo amewataka wafanyabiashara kuendelea kushirikiana na Serikali katika kukuza sekta ya biashara Wilayani hapa.
Wafanyabiashara waliohudhuria katika kikao hicho ni Pamoja na wafanyabiashara wa mahoteli, Zahanati, Maduka ya vyakula Pamoja na wafanyabiashara wengine
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.