Baraza la Madiwani la Manispaa ya Mtwara-Mikindani leo desemba 8, 2020 limemteua Diwani wa Kata ya Mtonya (CCM) Mhe. Shadida Ndile kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa baada ya kupata kura ishirini na tatu kati ya kura ishirini na tano zilizopigwa.
Kwa upande mwingine Diwani wa Kata ya Vigaeni Mhe. Saidi Ally Nassoro (CCM) amechaguliwa kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kupata kura ishirini na nne kati ya kura ishirini na tano zilizopigwa.
Menejiment ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani pamoja na watumishi tunawapongeza Madiwani hawa kwa nafasi walizopata na tuna ahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.