Mkuu wa Wilay aya Mtwara Mhe.Dunstan Kyobya amewataka wanavikundi waliopata fedha za mkopo wa asilimia 10 usio na riba kutoka Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuhakikisha wanalipa mkopo huo kwa hiyari na kwa wakati ili ziweze kuwasaidia watu wengine
“ Nimewaona hapa leo mnafuraha kupokea fedha zenu, niwasihi ndugu zangu kwa furaha hizi hizi mlizonazo leo kwenye kupokea fedha na muwenazo hata kwenye kufanya marejesho,fedha hizo ni za mzunguko lipeni ili na wengine wapate kukopa.msisubiri halmashauri iwafuate kwenye maeneo yenu’amesisitiza Mhe. Kyobya
Mkuu wa Wilaya ameasemahayo Desemba 2022 kwenye hafla ya kukabidhi mikopo kw avikundi 35 vya wananwake, vijana na watu wenye ulemavu iliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa
Katika kuhakikisha kuwa biashara za wanavikundi hao zinafanya vizuri Mkuu wa Wilaya amewataka wafanye biashara kidijitali kwa kutumia simu zao na kutangaza biashara kwenye mitandao ya kijamii ili waweze kuapta wateja wengi Zaidi.
Aidha ameiomba idara ya maendeleo ya jamii kuwasiliane na wataalamu kutoka SIDO ili wawape mafunzo yatakayoweza kuboresha bidhaa zao ili ziwe za kisasa Pamoja na kufuatilia kazi zao kwa ukaribu na kuzitangaza ili kila mtu kazi yake ionekane.
Mkuu w aWilaya amewataka wananvikundi hao kuimarisha umoja na mshikamao kwenye kutangaza biashara zao nndani na kujieppusha na ugomvi baina yao huku akiwataka madiwani kila mmoja kwenye kata yake kuhakikisha anafuatilia urejeshaji wa mikopo.
Aidha ameipongeza Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kutoa mkopo ndnai ya miezi mitano tangu mwaka mpya wa bajeti ulionza
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.