MWALIMU NYANGE NA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI WAUNGANA KUCHIMBA MSINGI JENGO LA UTAWALA TANDIKA
Ni muendelezo wa Msalagambo wa tatu katika mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Tandika ambapo Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange ameungana na wanafunzi 402 kutoka katika shule tano za Sekondari zikiwemo Mtwara Ufundi, Umoja, Rahaleo, Shangani na Sabasaba kuchimba msingi wa jengo la Utawala la mradi huo.Leo Agosti 11,2024.
Akizungumza mara baada ya mapumziko ya chakula kilichoandaliwa kwa ajili ya wanafunzi katika eneo la mradi huo, Mwalimu Nyange amesema kuwa lengo la kuwashirikisha wanafunzi hao ni kutaka kuwajengea dhana ya elimu ya uzalendo kwa Taifa lao.
Amesema kuwa ataendelea kuhamasisha watumishi, wananchi hususani vijana kujitolea ili waweze kuona kuwa kazi ya ujenzi wa Taifa ni shirikishi na sio kutegemea Serikali pekee.
Aidha amewapongeza wananchi husani wananchi wa Kata hiyo kwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki kusaidia juhudi za Serikali yao kwa kuchimba na kuweka zege katika mradi wa huo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.