Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeendelea kuviwezesha na kuviinua kiuchumi vikundi 58 vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kwa kuwapatia mkopo wa asilimia kumi usiokuwa na riba kiasi cha Shilingi milioni mia sita arobaini laki tisa themanini na tano (640,985,000), ambapo vikundi vya wanawake 33 vimepata mkopo wa shilingi 320,000,000, vikundi vya vijana 22 (313,085,000) na vikundi vya watu wenye ulemavu 3 (8,000,000) Leo Januari 6,2025
Akisoma taarifa kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Judith Palangyo amesema kuwa Manispaa ilipokea maombi 190 ya mkopo kutoka kwenye mfumo wa utoaji mikopo yenye thamani ya shilingi 3,450,853,080, ambapo kati ya maombi hayo wanawake walikuwa 126 wenye maombi ya mkopo wenye thamani ya shilingi 1,872,580,000, vijana 58 (1,549,130,500) na watu wenye ulemavu 6 wenye maombi ya mkopo wa thamani ya shilingi 29,630,000.
Amesema kuwa baada ya kupokea maombi hayo, Manispaa ilifanya upembuzi yakinifu kwa kutembelea kila mradi kwa kila kikundi na kufanya tathmini kwa kuzingatia uhalisia wa miradi na kiasi cha fedha kilichoombwa ambapo ilibaini kuwa katika vikundi 190 vilivyoomba mkopo ni vikundi 130 vikiwemo vya wanawake 105, Vijana 22 na watu wenye ulemavu 3 vilikidhi vigezo vya kupatiwa mkopo wa Shilingi 1,065,447,000.
Ameendelea kufafanua kuwa kutokana na maombi kuwa mengi kuliko fedha iliyopo, Manispaa imeanza kutoka mkopo wa awamu ya kwanza ambapo mkopo uliotolewa unaanzia shilingi 1,500,000 hadi shilingi 56,000,000.
Aidha Palangyo amesema kuwa vikundi vyote vinavyopata mkopo vimeshapewa mafunzo juu ya wajibu wa vikundi,uwekaji wa akiba pamoja na usimamizi wa fedha na mali za kikundi huku akiwasisitiza wanakikundi hao kuwa waaminifu na mfano wa kuigwa katika urejeshaji mzuri wa mikopo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.