Wakati tukisherehekea miaka 61 ya Uhuru leo 9 Desemba Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Dunstan Kyobya amekabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 244,869,000 ikiwa ni mkopo wa asilimia kumi usio na riba kwa vikundi 35 vya wajasrimali vilivyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani vikiwemo vikundi vya wanawake 24 (157,248,000), vijana 4 (60,411,000) na watu wenye ulemavu 7 (27,210,000) vyenye wanufaika wapatao 75.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Jemson Mwampiki amesema kuwa mwezi oktoba 2022 halmashauri ilipokea maombi ya mkopo ya vikundi 52 yenye thamani ya shilingi 503,972,000 na baada ya kufanya uhakiki vikundi 48 vilikidhi vigezo vya kupata mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 367,709,0000.
Aidha kutokana na upungufu wa fedha vikundi 13 vyenye thamani ya shilingi 116,840,000 vitapatiwa mkopo kwa awamu nyingine kwa kadiri fedha zitakavyokuwa zinapatikana .
Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeendelea kutii na kuzingatia agizo la serikali la uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani ikiwa ni 4% wanawake, 4% vijana na 2% kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha biashara zao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.