Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imeshika Nafasi ya Kwanza Kwenye Usimamizi wa Utekelezaji wa shughuli za lishe Mkoani Mtwara ikiwa ni mara ya tatu mfululizo kati ya halmashauri tisa zilizopo na kutunukiwa cheti cha pongezi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Leo Agosti 20,2024 katika Kikao Cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa usimamizi wa afua za lishe Kwa mwaka 2023/2024
Halmashauri imeshika nafasi hiyo baadae ya Kufanya vizuri Kwenye Utengaji na utoaji wa fedha za lishe kupitia mapato ya ndaji , Utoaji wa vidonge vya kuongeza wekundu wa damu kwa kina mama wajawazito, utoaji wa matibabu ya utapiamlo mkali kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 sambamba na Utekelezaji wa maadhimisho ya siku ya afya na lishe ngazi ya mitaa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.