Kutokana na kupungua kwa kesi za mashauri ya kinidhamu dhidi ya watumishi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Afisa kazi kutoka Ofisi ya kamishina wa kazi Mkoa wa Mtwara ndugu Selemani Seng’enge amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko kwa kusimamia vizuri nidhamu za watumishi.
AMetoa pongezi hizo Februari 26,2021 katika mkutano wa baraza la wafanyakazi uliofanyika katika Chuo Cha Ualimu Kawaida.
Amesema kuwa katika Ofisi yao wamekuwa wakipokea mashauri mengi ya kinidhamu ya watumishi kutoka sehemu mbalimbali jambo ambalo ni tofauti na Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Kwa namna nyingine Seng’enge amempongeza tena Mkurugenzi kwa kutoa ruhusa kwa watumishi kujiendeleza kimasomo bila kuwawekea vikwazo.
Aidha amewataka watumishi kufanya kazi kwa bidi ili halmashuari iweze kupata matokeo mazuri Zaidi.
Katika mkutano huo uliohusisha wafanyakazi kutoka Idara na Vitengo vyote wafanyakazi wamepata nafasi ya kuchagua wajumbe wapya wa baraza la wafanyakazi baada ya baraza lililopo awali kumaliza wake.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.