Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya akikabidhi bodaboda sita kwa vikundi viwili vya vijana vya Umoja na Kijana Jitume (Kata ya Shangani) ikiwa ni sehemu ya mkopo walipatiwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Katika kuhakikisha kuwa wananchi wanawezeshwa kiuchumi ili waweze kujiongezea kipato na kujikimu kimaisha Manispaa ya Mtwara-Mikindani kupitia mapato yake ya ndani imetoa mkopo wa shilingi Milioni 257.1 kwa vikundi 56 vya wajasiriamali wakiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi hundi ya mkopo kwa vikundi hivyo iliyofanyika Juni 12,2020 katika viwanja vya Ofisi za Manispaa, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amempongeza Mkurugenzi kwa kutii agizo la Serikali la kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwakopesha wajasiriamali.
Pamoja na pongezi hizo Kyobya pia amevitaka vikundi vilivyopatiwa mkopo kutumia fedha hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa ili waweze kurejesha fedha kwa wakati na wengine waweze kunufaika.
“Hii sio pesa ya kwenda kununua nguo, hii sio pesa ya kwenda kununua nyumba, huu ni mkopo unaosaidia kujikwamua kimaisha ,ukikopa lazima ulipe kwa wakati”alisema Kyobya
Kyobya pia amesisitiza kupelekewa mahakamani kwa wale wote watakaoshindwa kurejesha mikopo na kuwataka vijana kukaza buti ili waweze kurejesha mkopo waliopewa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Miindani Col. Emanuel Mwaigobeko amesema kuwa ana Imani mkopo uliotolewa kwa wajasiriamali haoutawasaidia ,kujiajiri Pamoja na kuyafanya Maisha yao kuwa bora.
Awali akisoma taarifa ya utoaji wa mikopo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii Bi Juliana Manyama amesema kuwa mkopo umetolewa kwa vikundi vya wanawake 42 vyenye mkopo wa wa shilingi 175,100,000, watu wenye ulemavu vikundi 3 vyenye mkopo wa shilingi 7,500,000 na Vijana vikundi 11 vilivyopata mkopo wa shilingi 74,500,000 na bodaboda 6 na kufanya idadi ya vikundi vilivyopata mkopo kuwa 56.
Ameongeza kuwa Katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 Manispaa ya Mtwara-Mikindani imekopesha shilingi 447,100,000 kwa vikundi 80 vya wajasiriamali vikiwemo vikundi vya wanawake 47, Vijana 27 na watu wenye ulemavu vikundi 6.
Pamoja na fedha zilizokopeshwa pia katika bajeti yake ya 2019/2020 halmashauri imepekea kwenye mfuko wa wanawake, Vijana na walemavu shilingi Milioni 339,000,000 sawa na asilimia 100 ya kiasi kinachotakiwa kuchangia katika mfuko mfuko wa vikundi.
Wakati huo huo Saidi Chinamenga Mjasiriamali wa kuuza genge amepokea kwa furaha mkopo huo na kuishukuruSerikali ya awamu ya tano kwa kuwaenzi walemavu na ameahidi kufanya kaiz kwa bidi ili aweze kurejesha mkopo kwa wakati.
Nae Podensiana Sungura mfugaji wa kuku amesema kuwa mkopo walioupata utasaidia kukuza mtaji wao na kuweza kulea familia zao na ameaasa waliochukua mkopo kurejesha kwa wakati.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.