Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amezindua ligi ya mpira wa miguu Ndile MEYA CUP pamoja na viwanja vya michezo katika Taasisi ya utafiti wa mazao ya kilimo (TARI) vilivyopo katika Kata ya Naliendele Mkoani Mtwara , huku akisisitiza vijana kutumia fursa hiyo kuonesha vipaji vyao katika kutafuta njia ya kuelekea kwenye timu kubwa.
Hii ni fursa, tutumie fursa hii kuleta maendeleo katika Kata yetu na Mkoa wetu kwa ujumla, onesheni vipaji vyenu ili vionekane , Michezo hii italeta fursa nyingi hapa , watu watakula watakunywa , tutumie fursa hii kwa umakini ili mashindano haya yalete tija kwa kila mmoja wetu” Alisema Kyobya
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika tarehe 30/05/2021 katika viwanja vya TARI Naliendele, Kyoba aliwashukuru wadhamini mbalimbali walijitokeza na kutoa rai kwa wadau wengine kuendeleza uzalendo wa kudhamini michezo mbalimbali ikiwa ni njia moja wapo ya kuibua wachezaji wengi chipukizi.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara -Mikindani Bi. Shadida Ndile, amewashukuru wadhamini na wadau walijitokeza na amewataka wananchi wa Mtwara Mikindani kuwa wazalendo na kushiriki michuanao hiyo kwa amani na kuepuka vurugu na migongano isiyo ya lazima itakayopelekea uvunjifu wa amani wakati michuano hiyo ikiendelea.
"Sitegemei vurugu na migongano, nategemea mashindano ya amani, haya mashindano ni yetu, naomba tucheze kwa upendo na uzalendo, tukiharibu tutawafukuza wadhamini wenyewe, tujitahidi kuyalinda” Alisema Ndile.
Aliongeza kuwa badala ya kukaa kijiweni na kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya , vijana watumie fursa hii ili kuingia katika soko la ajira kwani ndoto yake kubwa ni kuona vijana hao wanafika mbali kimichezo na kuunda timu ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, kuingia katika timu ya Mkoa na hata kupata fursa nje ya nchi.
Mashindano hayo yamezinduliwa tarehe 30 , mei 2021 na yatamalizika tarehe 11, julai 2021 katika viwanja vya Nangwanda Sijaona vilivyopo Manispaa ya Mtwara- Mikindani .
Ligi hiyo itashirikisha timu za mpira wa miguu 18 zilizoundwa kutoka katika Kata 18 zilizoundwa kutoka katika Kata 18 zilizopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.