Katika kuhakikisha kuwa mradi wa uchimbaji visima viwili vya maji unaondelea katika Kata ya Magomeni na Ufukoni unatekelezwa kwa wakati na katika viwango vilivyokubalika, Septemba 20,2021 Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassani Mtenga amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo na kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wake.
“Nimeridhishwa na kasi ya utekelezaji, hiki kisima cha Mbae kimechimbwa mita 53 hadi sasa na kile cha Ufukoni kimemalizika kwa kuchimbwa mita 100 tunasubiri hatua nyingine sasa” Amesema Mhe. Mtenga
Aidha Mhe. Mtenga amewataka wanananchi wa maeneo hayo kuahakikisha wanaimarisha ulinzi wa visima hivyo pindi vitakapoanza kufanya kazi.
“Visima hivi vimegharimu fedha nyingi sana hakikisheni mnaimarisha ulinzi, mnaona adha mnayoipata kwa sasa” Amesema Mhe. Mtenga
Ikumbukwe kuwa Agosti 29, 2021 Mhe. Mtenga alizindua mradi wa Uchimbaji wa visima 30 vya maji unaotekelezwa katika vijiji 30 vilivyopo katika Majimbo kumi Mkoani Mtwara ikiwemo visima hivi viwili vilivyotembelewa leo nfani ya Manispaa yetu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.