Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara - Mikindani Mhe. Shadida Ndile amezitaka Mamlaka zinazosimamia mchakato wa utoaji talaka zihakikishe zinaweka makubaliano ya wazi ya uwajibikaji baina ya wazazi ili kupunguza wimbi la watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
“Talaka isiwe sababu ya kufanya watoto wakose malezi, nitoe wito kwa Mamlaka husika simamieni makubaliano ya uwajibikaji baina ya wazazi” Amesema Mhe. Ndile
Ametoa rai hiyo Agosti 19 , 2021 katika hafla iliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Faidika Wote Pamoja (FAWOPA) ilipokabidhi vifaa vya shule kwa wanafunzi wa sekondari 67 na wanafunzi 11 wa chuo cha maendeleo ya jamii Mtawanya ambao wanaoishi katika mazingira magumu.
Amesema kuwa ukatili wa kutelekeza watoto umekuwa wa kawaida sana katika Jamii, talaka imekuwa njia ya wanandoa kukimbia majukumu yao na kupelekea watoto kukosa malezi na kuishi katika mazingira magumu.
Naye Mkurugenzi wa FAWOPA Baltazar Komba amesema kuwa kila mtoto ana haki ya kupata elimu na malezi bora ili kutimiza ndoto zake hivyo ni wajibu wa kila mzazi kuhakikisha mtoto wake anatimiza malengo yake aliyojiwekea.
Ili kufanikisha ndoto zao, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Bi. Juliana Manyama amewataka wanafunzi hao kutumia vizuri fursa waliopewa na FAWAPO kama daraja la kutimiza malengo yao.
Salum Khamis mwanafunzi wa Sekondari ya Sino ambae pia mnufaika wa msaada huo amelishukuru amelishukuru shirika hilo kwa misaada inayotoa na kuwaomba wadau wengine kujitokeza ili kuboresha ustawi wa elimu katika Manispaa Yetu.
Kwa kipindi cha miaka mitano shirika la FAWOPA limefanikiwa kuwasaidia wanafunzi 321 ambao wameunganishwa na taasisi za kielimu, na baadae wakaweza kujiajiri.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.