Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange amewaagiza Watumishi wapya wa Halmashauri hiyo kuwa waadilifu na kujiamini katika utendaji wao ili kuendana na kasi itakayoleta mchango chanya katika muda wao wa Utumishi.
Amesema Utumishi wa Umma kwao ni fursa muhimu ya kujijenga kiutendaji na kuacha alama katika Utumishi, ili waweze kukumbukwa kwa daima na kuisaidia Halmashauri hiyo kufikia malengo yake.
Ameongeza kuwa ni vema wakatambua kwamba nafasi walizopata ziligombewa na wahitaji wengi hivyo kwa wao kupata ni fursa nzuri sasa kuonesha kwamba haikua bahati kuchaguliwa wao bali walistahili.
Aidha, Mwalimu Nyange amewaahidi kuwapa ushirikiano watakaouhitaji katika kipindi chote cha utumishi wao ili Halmashauri iweze kufikia malengo tarajiwa.
Jumla ya watumishi wapya 41 wamefaulu na kupata ajira katika usaili uliofanyika mapema mwezi huu (Oktoba), katika kada za Watendaji wa Mitaa, Madereva, Waandishi waendesha Ofisi pamoja na Wasaidizi wa kumbukumbu.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.