Mbunge wa jimbo la Mtwara Mjini Mhe.Hassan Mtenga kwa kushirikiana na bank ya CRDB , Agosti 4,2021 amefanya kikao na madereva wa pikipiki (bodaboda) wa Manispaa ya Mtwara – Mikindani ili kuwapa maelekezo ya upatikanaji wa mkopo wa pikipiki utakaotolewa na benki hiyo hapo baadae.
Mtenga maesema kuwa katika kampeni za kugombea Ubunge alihaidi kuwapatia fursa bodaboda hao ikiwemo Mikopo na kwamba leo hii anatimiza ahadi yake kwa kushirikiana na CRDB.
Sambamba na maelekezo hayo, Mhe. Mtenga amewakata madereva hao kuzingatia sharia na kanuni za uendeshai wa vyombo vya moto lakini pia kuboresha utoaji wa wa huduma zao ili kujiongezea kipato na kupanua wigo wa biashara .
“Huduma ya wateja nzuri ndio itawapa sifa kubwa zaidi, ukimuhudumia mteja leo lazima atakuwa balozi huko anakoenda, vaa vizuri na kuwa na lugha nzuri utaona biashara yako itasimama”Amesema Mhe.Mtenga
Ili derva aweze kupata mkopo huo anatakiwa kuchangia 20% ya bei wakati wa ununuzi wa pikipiki, awe na mdhamini ambae mshahara wake unapitia Benki ya CRDB lakini pia awe na leseni inayomruhusu kuendesha bodaboda
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.