Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara Ndugu Mgeni Musaa Haji ameridhishwa na kasi nzuri ya ujenzi w amadarsa ya Sekondari yanayoendelea kujengwa katika Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani na kuupongeza Uongozi mzima wa Mnaispaa kwa juhudi hizo.
“Nikupongeze Mkuu wa Wilaya na timu yako kazi inaenda vizuri, kasi ya ujenzi imekuwa kubwa ni matumaini yangu tutakabidhi madarsa haya mapema “alisema Mgeni
Katibu Mgeni ametoa pongezi hizo leo Desemba 2,2021 alipofanya ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Manispaa yetu na kukagua madarasa kumi na nne kati ya madarasa ishirini na mbili yanayoendelea kujengwa.
Ameendelea kuwasisitiza wakuu wa Shule kuwashirikisha wananchi pale fedha za ujenzi wa madarsa zitakapobaki na kuzipangia matumizi mengine.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ameahidi kuw ahadi kufikia Desemba 5, 2021 Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani tutakuwa tumeshakmailisha ujenzi w amadarasa ishirini na mbili ya Sekondari na kukabidhi kwa Mkuu wa Mkoa..
Shule zilizotembelewa ni Pamoja na shule ya sekondari ya Mitengo, Sino, Chuno, Mtwara Ufundi na Shangani.
Manispaa ya Mtwara-Mikindani imepokea fedha za Mpango wa Maendeleo kw aUstawi wa Taif ana Mapambano Dhifdi ya UVIKO-19 shilingi Milioni 440 kw ajili ya ujenzi wa Madarsa ishirini nambili ya Sekondari
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.