Kamati ya Siasa Mkoa Mtwara imepongeza Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika sekta ya Elimu na Afya kwa kuendana na thamani ya fedha zilizotengwa.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Ndugu Mobutu Malima, wakati wa majumuisho ya Ziara ya kawaida ya kukagua Miradi inayotekelezwa kupitia Ilani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika leo tarehe 08/01/2025.
“Kwa namna tulivyokagua miradi hii, tumeona tumeridhika kwa kweli ni mizuri, hongereni sana! Tumeona thamani ya fedha,” alisema Malima.
Ndugu Malima aliongeza kuwa ubora wa majengo yote yaliyokaguliwa imeendana na thamani ya fedha na akasisistiza watendaji na wataalamu kuendelea kutanguliza uzalendo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha, alisisitiza Manispaa hiyo kuongeza kasi kwenye umaliziaji wa miradi iliyokatika hatua za mwisho kukamilika hususani katika ujenzi wa hospitali ya Wilaya iliyopo Mjimwema kata ya Magengeni.
Sambamba na hilo, Ndugu Malima alitumia ziara hiyo kujitambulisha kwa Watumishi wa Manispaa hiyo huku akitoa rai juu ya kuzingatia namna ya utekelezaji wa ilani wa chama tawala.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdalah Mwaipaya, akitoa salamu zake alisema ziara hiyo ni ya kawaida kwaajili ya kukagua miradi inayotekelezwa chini ya Ilani ya CCM na akawapongeza wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa serikali katika utekelezaji wa ilani hiyo.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mwalimu Hassan Nyange, alis
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.