Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bi. Edith Shayo amesema kuwa watendaji wa halmashauri wanatakiwa kujipanga kuandika maandiko ya kuomba fedha za miradi yenye tija na kupeleka maandiko hayo Serikali kuu ili waweze kuleta fedha za utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuwa hazina imesema kuwa ina fedha za kutosha.
Shayo ameyasema hayo Leo Mei 26,2023 kwenye Mkutano wa baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za halmashauri uliofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Kawaida uliopo Mnaispaa ya Mtwara- Mikindani.
Aidha amewasisitiza Madiwani na watendaji kuhakikisha wanafanya jitihada za kina za kuhakikisha wanashirikiana kwenye ukusanyaji wa mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuvifuatilia ili Manispaaa iweze kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi.
Sambamba na hilo Shayo amewasisitiza watendaji kuhakikisha wanajitahidi kumaliza hoja za ukaguzi na ikibidi hoja zitakazobaki ziwe za kisera tu huku akiwakumbusha watendaji wanapofanya kazi zao mara zote kuhakikisha wana kuwa makini kutosababisha hoja za ukaguzi ambazo zinaleta taswira mbaya kwenye halmashauri.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.