Katika kuhakikisha kuwa madeni ya kodi ya ardhi yenye thamani ya shilingi Bilioni tatu kwa Manispaa ya Mtwara-Mikindani yanaendelea kulipwa, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya leo Januari 18,2020 amekutana na wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi kwa lengo la kuwaelimisha na kuwahamasisha ili waweze kulipa kodi hiyo.
Katika kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara Kyobya amewataka wadaiwa wakodi hiyo kuhakikisha wanailipa ifikapo Januari 30 mwaka huu.
Aidha ametoa wito kwa Manispaa kuhakikisha kuwa inarekebisha taarifa za ukusanyaji wa kodi ya ardhi zilizopo kwenye mfumo ili kila mmoja alipe kodi anayostahili.
Sambamba na hilo kyobya pia ametoa hamasa kwa wamiliki wote wa viwanja kuhakikisha wanasafisha maeneo yao ili kuondoa vichaka vinavyosababisha uhalifu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko amesema kuwa Taasisi nyingi za Serikali na dini zinadaiwa fedha nyingi zipatazo shilingi Bilioni 7.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.